Isaiah 21:6-9

6 aHili ndilo Bwana analoniambia:

“Nenda, weka mlinzi,
na atoe taarifa ya kile anachokiona.
7 bAnapoona magari ya vita
pamoja na kundi la farasi,
wapanda punda au wapanda ngamia,
na awe macho, awe macho kikamilifu.”
8 cNaye mlinzi alipaza sauti,

“Mchana baada ya mchana, bwana wangu, ninasimama katika mnara wa ulinzi,
kila usiku ninakaa mahali pangu nilipoamriwa.
9 dTazama, yuaja mtu anayepanda gari la vita
pamoja na kundi la farasi.
Naye anajibu:
‘Babeli umeanguka, umeanguka!
Vinyago vyote vya miungu yake
vimelala chini vikiwa vimevunjwa!’ ”
Copyright information for SwhNEN